Availability: Out of Stock
STADI ZA KISWAHILI : SHUGHULI ZA LUGHA GREDI 3
SKU: 9789966630421
Kshs 365.00
Stadi za Kiswahili, Kitabu cha Mwanafunzi, Gredi ya 3 ni kitabu cha kiada kilichoandaliwa kwa mujibu wa mtaala mpya uegemeao umilisi uliozinduliwa na
Taasisi ya Ukuzaji Mitaala ya Kenya (KICD) mnamo Septemba 2017.
Kitabu hiki kimejumuisha mada zote kuu na ndogo zilizomo katika ruwaza ya mtaala ya Kiswahili cha Gredi ya 3. Isitoshe, mada kuu na ndogo zimepangwa kulingana na jinsi zilivyopangwa katika ruwaza hiyo.
Fauka ya haya, yaliyomo yamewasilishwa kwa ubunifu wa hali ya juu ili kuyaoanisha na umilisi wa kimsingi, masuala mtambuko, maadili miongoni mwa masuala mengine yanayofumbatwa na mtaala mpya uegemeao umilisi.
Kitabu hiki kimejumuisha shughuli za aina nyingi za kufanywa na mwanafunzi binafsi, wanafunzi wawiliwawili na makundi ya wanafunzi. Kazi na shughuli za wanafunzi wawiliwawili na wanafunzi katika makundi zinadhamiriwa kuimarisha stadi za kusikiliza na kuzungumza na vilevile umilisi wa ushirikiano na mawasiliano.
Aidha, kitabu hiki kimesheheni vifungu vya kusoma na vya kuchangamsha vitakavyomsaidia mwanafunzi kuimarisha stadi ya kusoma. Stadi ya kuandika haijaachwa nyuma. Kitabu kinazo shughuli za kutosha za mwanafunzi ili kustawisha stadi ya kuandika.
Kwa mintarafu hii, kitabu hiki kitamwezesha mwanafunzi wa Gredi ya 3 kuwasiliana kwa Kiswahili sanifu katika mazingira mbalimbali yanayoshughulikiwa katika mada kuu.
ISBN : 9789966630421
Published : N/A
Author : Mwalimu Kipande
Language : Swahili
Main Material : Paperback
Publisher : Moran (E.A.) Publishers Limited
Size :
Weight : N/A
Out of stock
Sign in
Create an Account
Shopping cart
close