ANASA BY YUSUF KINGALA
Kshs 490.00
Yusuf M. King’ala alizaliwa mwaka wa 1 951 katika kijiji cha Makuthuni (Oldonyo Sabuk) Wilayani Machakos. Alisomea Oldonyo Sabuk HGM, Starehe Boys’Centre na Kenyatta University College ambapo alijipatia shahada ya Bachelor of Education Hons—1978. Hivi sasa ni mwalimu wa Kiswahili katika shule ya Starehe Boys’Centre.
Bwana King’ala si mgeni katika uwanja wa fasihi. Ni mwandishi wa vipindi vya fasihi vinavyotayarishwa na Taasisi ya Elimu ya Kenya. Ameshawahi kuchapisha vitabu viwili. Anasa ni kitabu chake cha tatu kuchapishwa.
Hawa, msichana mbichi ambaye anaendelea vyema na masomo yake anashikana urafiki wa kimapenzi na Mzee Tamaa. Urafiki huu ambao umejaa anasa, unafikia kikomo baada ya Hawa kutambua kuwa yu mja mzito. Hawa anakimbilia mjini ambako anaajiriwa kazi katika bar. Anasa anazaliwa katika mazingira mabaya ambayo yanamfanya kuwa mwehu. Mwisho Anasa anakuwa jambazi, mhalifu na mwizi stadi. Baada ya mikasa kadha ya uhalifu Anasa ananaswa na kuhukumiwa kunyo-ngwa. Swali ni hili: Ni nani hasa mwenye hatia katika hadithi hii?
ISBN : 9789966462039
Out of stock