Availability: In Stock

NYOTA YA KISWAHILI KITABU CHA MWANAFUNZI GREDI YA PILI

SKU: 9789966511089

Kshs 345.00

Kitabu hiki kimedhamiriwa kutumika kama mfululizo wa vitabu vya kiada kwa Gredi ya Pili. Kimeandikwa kuambatana na mtalaa mpya. Kitabu hiki kimelenga kumwongoza mwanafunzi katika masomo yake ya lugha ya Kiswahili kwa kutimiza maarubu ya mtalaa wa kiwango husika. Ndani yake mna mbinu bora za ujifunzaji ambazo zitawaelekeza wanafunzi kuhusu njia bora za kutimiza malengo yao.

Kimezingatia stadi zote za kujifunza lugha, yaani:

  • Kusikiliza
  • Kuzungumza
  • Kusoma
  • Kuandika
  • Msamiati
  • Sarufi
    • Mwanafunzi amepewa nafasi ya kujifunza mwenyewe kutokana na picha maridhawa, hadithi, mashairi na michezo murua. Ili kuzidisha hamasisho la ujifunzaji, mwongozo maalumu umeandaliwa ili kuwapa walimu mbinu thabiti za kuuchochea ujifunzaji miongoni mwa wanafunzi. Ili kutathmini kiwango cha ujifunzaji miongoni mwa wanafunzi kitabu hiki kimetoa mazoezi ya kutosha yatakayowawezesha kupata:

      • Umilisi wa kimsingi
      • Maadili ya kimsingi
        • Uwezo wa kuyashughulikia masuala mtambuko Zaidi ya hayo uchochezi huo huwafahamisha namna ya kulinganisha uhusiano wa mada waliyojifunza;

          • na masomo mengine
          • na shughuli za huduma za kijamii zinazochangia ujifunzaji
          • na shughuli nyingine zilizoratibiwa za ujifunzaji
            • Kitabu hiki kimeandikwa na waandishi wenye tajiriba pevu. Wamekomaa kwenye stadi ya uandishi wa vitabu vya kiada.

ISBN : 9789966511089

Published : N/A

Language : Swahili

Main Material : Paperback

Publisher : The Jomo Kenyatta Foundation

Size :

Weight : N/A

132 in stock