SAUTI NA MAZOEZI YA KISWAHILI GREDI 2
Kshs 445.00
Sauti na Mazoezi ya Kiswahili, Gredi 2 ni kitabu cha ziada kilichotungwa ili kumpa mwanafunzi shughuli na mazoezi ya
kutosha hasa kuhusiana na sauti za Kiswahili. Mazoezi ya sauti yamepewa nafasi kubwa ili kumwezesha mwanafunzi
kutambua herufi za alfabeti na sauti zinazowakilishwa na herufi hizo. Utambuzi huu ni msingi muhimu katika
umilisi wa stadi za kusikiliza na kuzungumza, kusoma na kuandika. Mtaala mpya uegemeao umilisi umetambua pengo hilo.
Ndiyo sababu umetenga orodha ya sauti zinazopaswa kushughulikiwa katika kila gredi. Kitabu hiki kimetungwa kujaza pengo hilo.
Hata hivyo, lugha ni muhimu ifundishwe katika ukamilifu wake. Kutokana na ukweli huu, kitabu hiki kimejumuisha mazoezi
katika mada zote kama zinavyopendekezwa na mtaala mpya uegemeao umilisi. Katika kitabu hiki, mwanafunzi anahusishwa:*
kutamka sau?i, silabi na maneno .kuunganisha na kutenganisha silabi katika manenoti
• kujaza mapengo
• kupanga maneno yaliyo na sauti fulani katika orodha
• kuunda maneno kutokana na majedwali ya silabi.
• * kubaini maneno yaliyo na sauti zinazoshughulikiwa 3 * kuchora na kupaka rangi
• kutafuta maneno katika mirabakujaza miraba
• kusoma na kujibu maswali ya hadithi kuandika mambo yanayoonekana katika picha, kutazama na kusimulia kuhusu picha
kutazama na kuchambua picha kuambatanisha majina na picha …miongoni mwa shughuli nyingine za kuchangamsha.
ISBN : 9789966631916
Published : N/A
Language : Swahili
Publisher : Moran (E.A.) Publishers Limited
Size :
Weight : N/A
4 in stock