Vitendawili vya Kikwetu (riddles)
Kshs 480.00
KlTABIi HIKI KINA VITENDAWILI 1180 NA MAJIBU YAKE YALIYOTOLEWA KWA N|IA YA PICHA
Matumizi ya picha kutoa majibu ya vitendawili ndiyo namna halisi inayopaswa kutumika ili kufundishia watoto na vijana vitendavvili. Hii ni kwakuwa picha zitawasaidia wasomaji wadogo kufahamu maumbile halisi ya vitu mbalimbali ambavyo pengine hata havipo kwenye mazingira yao ambavyo ndivyo majibu ya vitendawili.
Zaidi ya kuwajengea wasomaji utambuzi wa vitu mbalimbali, matumizi ya picha katika kutoa majibu ya vitendawili yatamwongezea msomaji ufahamu wa maneno mengi muhimu ya Kiswahili. Kwa kutumia kitabu hiki msomaji atajifunza maneno zaidi ya 700 ambayo yatamwongezea uwezo wake wa kutumia Kiswahili kujieleza kwa ufasaha na kwa vionjo. Baadhi ya maneno muhimu kabisa ambayo hayajazoeleka yanayopatikana katika kitabu hiki ni kama: njuga, dema, kokochi, zumari, mbinja, uboho, kope, kingo, ulimbo, istiwai na mwega. Maneno haya na mengine mengi yatamsaidia msomaji kuifahamu na kuweza kuitumia Lugha hii vema zaidi.
ISBN : 9789987701322
Published : N/A
Author : H. D. Salla
Language : Swahili
Main Material : Paperback
Publisher : APE Network
Size :
Weight : N/A
207 in stock